Wananchi Waalikwa Kutembelea Mabanda ya IAA Maonesho ya Nanenane

Chuo Cha Uhasibu Arusha IAA kinashiriki Maonesho ya NaneNane mwaka 2024 katika Kanda ya Kaskazini katika Viwanja Vya Themi Njiro Jijini Arusha, Kanda ya Kati Viwanja vya Nzunguni Jijini Dodoma na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Viwanja Vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Wananchi wanaalikwa kutembelea mabanda ya IAA katika Kanda zote tatu ili waweze kupata huduma mbalimbali ikiwemo; jufanya udahili wa wanafunzi bure, kupata taarifa za kozi mbalimbali, pamoja na kupata ushauri wa kujiunga na kozi mbalimbali kulingana na ufaulu wa mwanafunzi

Aidha, wananchi watapata fursa ya kuona kazi za ubunifu, uvumbuzi na biashara zinazofanywa na wanafunzi wa IAA wanaolelewa chini ya kiotamizi( IAA Business Startup Centre -IBSUC)) ambao wamewezeshwa kuanzia kwenye uandishi wa mawazo ya biashara mpaka kusajili kampuni zao wakiwa chuoni.

Kauli mbiu ya Maonesho ya Nanenane kwa mwaka 2024 ni “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa Kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.